Genesis 27:37-40

37 aIsaki akamjibu Esau, “Nimemfanya yeye kuwa bwana juu yako, pia nimewafanya ndugu zako wote kuwa watumishi wake, nimemtegemeza kwa nafaka na divai mpya. Sasa nitaweza kukufanyia nini, mwanangu?”

38 bEsau akamwambia baba yake, “Je, baba yangu una baraka moja tu? Unibariki mimi pia, baba yangu!” Kisha Esau akalia kwa sauti kubwa.

39 cBaba yake Isaki akamjibu, akamwambia,

“Makao yako yatakuwa
mbali na utajiri wa dunia,
mbali na umande wa mbinguni juu.
40 dUtaishi kwa upanga,
nawe utamtumikia ndugu yako,
lakini wakati utakapokuwa umejikomboa,
utatupa nira yake
kutoka shingoni mwako.”
Copyright information for SwhNEN